emergency-sign
Taarifa iliyonifikia muda mfupi uliopita inahusu ajali ya kuanguka kwa Jengo ambalo lilikuwa linaendelea kujengwa.
Mtu mmoja amefariki na wafanyakazi na wakazi wengine wa eneo la Ruaraka, Kenya wamenusurika kifo kutokana na ajali ya kuanguka kwa jengo ambalo lilikuwa linaendelea kujengwa, kwa mujibu wa mashuhuda wanasema ajali hiyo imesababishwa na nyufa zilizokuwa katika jengo hilo.
Taarifa ya Citizen News imesema wakazi wa eneo hilo wamesema kwamba waliwahi kuwakemea wamiliki wa jengo hilo kwa kufanya ujenzi chini ya kiwango lakini hakuna mabadiliko yaliyowahi kufanyika.
Uchunguzi unafanyika kubaini sababu iliyopelekea ajali hiyo.
Wakazi wa eneo hilo wakiwa eneo la tukio lilipoanguka jengo hilo. Picha: Citizen News
Wakazi wa eneo hilo wakiwa eneo la tukio lilipoanguka jengo hilo. Picha: Citizen News

Soma Nafasi za kazi na ajira bofya hapa chini kutizama, Mjulishe na mwenzio

Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio

Post a Comment

 
Top