. Kocha
Juma Mwambusi ameuandikia barua uongozi wa Mbeya City ya kubwaga
manyanga kuinoa timu hiyo kwa kuchoshwa na kelele za shutuma dhidi yake.
Mbeya
City imeanza vibaya Ligi Kuu Bara msimu huu kwani inashika mkia ikiwa
na pointi tano baada ya kucheza michezo saba, imeshinda mmoja, imetoa
sare miwili na kufungwa minne.
Kufanya
vibaya kwa timu hiyo kumeibua maneno mengi hasa wakimtuhumu Mwambusi
kuwa ameshindwa kazi na ndio sababu uwez wa timu hiyo umeporomoka.
Kutokana
na jambo hilo, kocha huyo wa zamani wa Prisons ameamua kuachia ngazi
ili kuwapisha wengine baada ya kuchoshwa na maneno mengi yanayoelekezwa
kwake.
Mwamabusi
aliliambia gazeti hili jana kuwa ameamua kujiweka pembeni ili kuwapisha
makocha wengine watakaoweza kuinoa timu hiyo na kuipa mafanikio.
“Maneno
ni mengi sana baada ya matokeo haya na wengi wanaelekeza maneno haya
kwangu kuwa sifai, mimi mkali, hivyo nimeona bora niwaachie timu yao ili
kulinda heshima yangu.“Nimekaa
na timu hii kwa miaka minne, nimeipandisha daraja, nimekaa na wachezaji
wangu vizuri na msimu uliopita tukafanya vizuri lakini msimu huu mambo
yamekuwa tofauti na maneno mengi yameongelewa, mengine yamehusisha
familia yangu,” alisema na kuongeza: “Leo naaambiwa eti mimi mkali ndio
sababu wachezaji wanashindwa kucheza kwa kiwango, lakini miaka yote
nimekaa na timu mbona sikuambiwa hivyo. Alipoulizwa katibu wa klabu
hiyo, Emmanuel Kimbe kama wamepokea barua ya kocha huyo, alisema hadi
wakati huo hakukuwa na barua ya Mwambusi.
|
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment