Kwenye
historia ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo kuna historia
nyingine inaandikwa ambapo Mbunge mwingine amefunga Ndoa.
Tumezoea Wabunge wetu wakipewa nafasi ya kuchangia jambo ndani ya kikao cha Bunge huwa wanaanza kwa pongezi, utasikia hivi; “.. Kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge au Waziri………”
Jumatatu kikao cha Bunge kitaendelea na nadhani hautoshtuka ikitokea Mbunge hata mmoja akisema hivi; “… Nimpongeze sana Mheshimiwa David Kafulila, Mbunge wa Kigoma Kusini kwa kufunga ndoa siku ya Jumamosi..”
Yes..
Ni kweli.. Mbunge huyo amefunga ndoa leo Kigoma, ujumbe alioandika
Zitto Kabwe kwenye ukurasa wake wa Facebook ni huu hapa; “..Bwana Harusi
David Kafulila akiwa na msimamizi wa ndoa yake Deo Filikunjombe na
marafiki zake David Silinde na Mwami..” halafu kuna picha aliyoiweka
akiwa na Wabunge hao.
Read more: http://jijiletuleo.blogspot.com/2014/11/mbunge-wa-kigoma-kaskazini-david.html#ixzz3Jryk6xJU
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment