Akichezesha taya na mwandishi wa habari hii, Shamsa alisema kuwa tangu alipoanza uhusiano na mchumba wake aitwaye Dick kisha kuzaa naye, walikuwa wamepanga wazae angalau watoto saba ila wapishane kidogo ili waweze kuwalea vizuri.
“Siwezi kutosheka kuzaa watoto wawili au watatu, nitakachofanya nitazaa mpaka basi. Sijali kwamba eti nikizaa nitachuja na kuharibu umbo langu kwani naamini kuwa hata kama nisipozaa bado umri utazidi kwenda na nitakapofikia kuzeeka nitazeeka bila kuwa na watoto,” alisema Shamsa.
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment