Ukimuona kwa macho utasema huyu ndio mwanamke kumbe ni bonge la kimeo…ilikuwa mida ya jioni natoka zangu kazini mara ikaingia massage..baby uko wapi nimekumiss…nikamjibu ndo natoka kazini now..yeye..Basi naomba upitie nyumbani japo nikuone nimekumiss sana we mwanaume.
Nikaona isiwe shida ngoja nikamuone roho yake itulie nipo njiani wazo likanijia…Nikapitia duka moja maarufu Sinza na kumnunulia zawadi ya viatu kama suprize nimejikoki mwenyewe naenda kwa babybaby…
mademu bwana..!
Kufika akanipokea kwa bashasha na mabusu motomoto dady’s home..Yeye.. najua umechoka baby wangu kaa kwa kochi upumzike nataka nikutengenezee juice fresh unayo ipendaga..nikamwambia ngoja kwanza nikupe zawadi yako nikatoa vile viatu na kumpatia akafurahi sana na kuvijaribisha..vilimtosha na kumpendeza..Nikapewa busu lingine la sekunde kazaa.,
Akatoka kwenda kuandaa juice..huku simu yake na vile viatu akiwa ameviacha jirani na kochi nililokaa..Nikamuuliza simu yako inabando..akanijibu ndio..Nikaichukua nakuingia sehemu ya kubrowse internent ..akili ikanituma nifanye udukuzi kidogo nikafungua application yake ya watsupp mbona nilichoka..
Nilikuta msururu wa wanaume anaochati nao nakuwatumiana picha akiwa amevaa pichu tu nakukaa kimitego…huku wakiambiana ni jinsi gani wamemisiana kupeana utamu..kijasho kikanitoka. .nikajikaza mwenyewe na kuendelea kuperuzi kwa wote idadi ikafikia wanaume kumi na moja na kwa mtiririko wa chating yao wote waonekana wameshapewa utamu..Napenda kusema kitu kimoja hapa tangu nimeanza mahusioano nae tumefikisha mwaka sasa sikuwahi hata siku moja kuishika simu yake.

Soma Nafasi za kazi na ajira bofya hapa chini kutizama, Mjulishe na mwenzio

Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio

Post a Comment

 
Top