AVictoria

Siku chache baada ya yule jamaa aliyevunja rekodi ya kutembea kwenye kamba umbali mrefu akiwa amefunga macho kwa kitambaa, leo kuna story ya hawa wengine ambao huenda rekodi yao ikawa ya kipekee pia kutokana na mazingira ambayo walifanikisha zoezi hilo.
Safari hii rekodi hiyo imevunjwa Afrika, ambapo Lukas Irmler kutoka Ujerumani na Reinhard Kleindl kutoka Austria walifunga safari na kuingia Afrika na kuvunja rekodi hiyo katika maporomoko maarufu ya Victoria Falls yaliyopo mpakani mwa Zambia na Zimbabwe.
0
Unaambiwa wakali hao walimaliza safari yao juu ya kamba umbali wa mita mia moja, ambayo iliisha salama mbali na changamoto ya upepo mkali pamoja na nguvu ya uvutano ya maji ambayo iliwafanya wayumbe lakini kilichowasaidia ni kuangalia mbele muda wote kitu ambacho hakikuwa rahisi.
cegrab-20141109-052515-0-1-362x204
Rekodi hii ni ya pili kuingia kwenye headlines, ambapo ya kwanza ilivunjwa Chicago Marekani na Nik Wallenda ambaye alijifunga kitambaa usoni na kutembea umbali wa mita 182 katika kamba iliyofungwa katika maghorofa mawili marefu.

Soma Nafasi za kazi na ajira bofya hapa chini kutizama, Mjulishe na mwenzio

Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio

Post a Comment

 
Top