Club hii imeripotiwa kumsajili kipa wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania Victor Valdez baada ya kufanya nae mazoezi kwa muda wa karibu mwezi mzima.
Valdez ambaye aliihama Barcelona baada ya mkataba wake kuisha msimu uliopita alikuwa karibu kujiunga na Liverpool lakini jeraha baya la goti alilopata katikati ya msimu uliopita lilizuia usajili wake kwenda Anfield.
Katika kipindi hiki kocha wa Manchester United Louis Van Gaal alimpa kipa huyo nafasi ya kufanya mazoezi na United hali ambayo ilimuweka karibu na usajili ndani ya klabu hiyo .
Usajili wa Valdez ulithibitishwa na kipa namba moja wa United David De Gea ambaye alizungumza na waandishi wa habari na kuwathibitishia kuwa United imemsajili Valdez.
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment