Unaweza
usiamini ama kufikiria kuwa kinyesi cha binadamu kina thamani kiasi cha
kutumika kama mbadala wa mafuta katika gari lakini unaambiwa Basi la
kwanza Uingereza linalotumia nishati hiyo limeingia barabarani.
Basi
hilo lenye uwezo wa kubeba abiria40 ‘Bio bus’ linatumia gesi itokanayo
na kinyesi cha binadamu na takataka nyingine zinazozalishwa kwenye
kiwanda kilichopo kusini Magharibi mwa nchi hiyo kuweza kutembea.
Katika
Gazeti la UHURU limeandika kuwa tanki moja la gesi hiyo lililozalishwa
kutokana na kinyesi cha watu inatosha kuendesha gari hilo kwa umbali wa
kilomita305.
Basi
hilo rafiki wa mazingira ambalo watengenezaji wake wanasema litaboresha
hewa, linaendeshwa kwa nishati ambayo ni ya kawaida,kinyesi cha
binadamu ambacho ni miongoni mwa majitaka mengine.
Watengenezaji
hao walisema gari hilo la aina yake litaboresha hali ya hewa na
kuthibitisha kumbe kuna thamani katika kinye si cha binadamu.
Zipo
taarifa kuwa siku si nyingi kinyesi cha binadamu kitaanza pia kuzalisha
nishati kwa ajili ya simu za mkononi baada ya wataalam kutoka chuo
kikuu cha East Anglia cha nchini humo.
Gesi
hiyo inazalishwa katika mtambo wa majitaka wa Wessex Water,unaendeshwa
na kampuni ya nishati ya Geneco na ugunduzi ,huo unaweza kuzalisha
nishati kwa ajili ya teknolojia inayobebeka kama vile simu za mkononi na
hata kompyuta mpakato.
Watetezi
wa nishati hiyo wanasema basi hilo ambalo linatarajia kusafirisha
abiria 10,000 kwa mwezi,linaonyesha thamani ya takataka na linaonyesha
mustakabali mwema katika sekta ya usafiri wa umma.
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment