Bwana
harusi mmoja kutoka Saudi Arabia amempa talaka mkewe siku ya harusi
baada ya kumuona uso wake kwa mara ya kwanza wakati mpiga picha
alipotaka kuwapiga picha.
Maharusi
hao kutoka mji wa magharibi wa Saudia,Medinah walikubaliana kuoana
licha ya kutoonana uso kwa uso,swala ambalo ni utamaduni mkubwa wa
mataifa ya mashariki ya kati.
Lakini
wakati mwanamke huyo alipofungua kitambaa alichokuwa amejifunika uso na
kutabasamu katika kamera,mumewe alishtuka na kuondoka wa ghafla.
Kulingana
na gazeti moja katika eneo hilo kwa jina Okaz,mwanamume huyo alianguka
na kuzirai huku wageni waalikwa wakijaribu kuingilia kati ili kutatua
kilichokuwa kikiendelea.
Hata hivyo Bwana harusi alisema kuwa hakuweza kumwona bi harusi kabla ya harusi yao gazeti hilo la Okaz liliripoti.
'' Si wewe msichana niliyetaka kuoa,si wewe kamwe niliyedhani '' kwa hivyo nakupa talaka''alisema bwana harusi.
Na alipompa talaka bi harusi naye alianguka na kuzirai na kuifanya harusi hiyo kuwa usiku wa majonzi.
via>>BBC
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment