Ripota wa bekamtanzania.com Elisa Shunda kutoka Dar es salaam ameziwasilisha hizi picha za wakazi wa kata ya Ubungo wakiwa katika msururu wakisubiri kupatiwa vitambulisho vyao vya uraia ambavyo vimekuwa ngumu kuvipata kutokana na mpangilio unaolalamikiwa kuwa mbovu wa mamlaka ya vitambulisho (NIDA).
Baadhi ya wananchi waliofika katika kituo hicho na vingine wamekuwa wakilalamika kutokuona majina yao katika picha na majina yanayobandikwa katika ukuta wa ofisi za mitaa na kata.
Wengine wanasema wafanyakazi wa Mamlaka ya vitambulisho vya taifa (NIDA) wamekuwa wakiwasaidia watu wengine kuwapatia vitambulisho kinyume na utaratibu jambo ambalo huwa linaleta msongamano mkubwa sana na kuwafanya wafanyakazi hao wasifanye kazi zao kwa ufanisi.
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment