Inasikitisha sana kifo cha huyu bwana Leonard Mtensa kilichotokea ndani ya gari lake, mpenzi wake anashikiliwa na polisi kwa uchunguzi zaidi. Hapa chini ni picha ya huyo dada na picha ya marehemu.

Jackline Hassan mwenye umri wa miaka 25 aliyekuwa na marehemu 

Huyu ndiye marehemu bwana Leonard Mtensa alikutwa na mauti ndani ya gari lake aina ya IST akiwa na mpenzi wake.
Jeshi la polisi mkoa wa Kagera linachunguza kifo cha ghafla cha Bw. Leornald Mtensa Stephen mwenye umri wa miaka  50 ambaye ni mmiliki wa club ya Lina's night club.

Tukio hilo la aina yake limetokea mnamo tarehe 18 mwezi huu majira ya saa nne usiku maeneo ya Buyekera manispaa ya Bukoba.

Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la polisi kwa vyombo vya habari ni kwamba Marehemu alikuwa anafanya mapenzi ndani ya gari lake lenye namba za usajili T982 CQG aina ya IST na mpenzi wake Jacline Hassan mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa Buyekera.
Wakati marehemu akiwa katikati ya tendo hilo ghafla hali yake ilibadilika na kukimbizwa katika kituo cha afya cha LCT NDOLAGE iliyopo Manispaa ya Bukoba na alifariki dunia wakiwa njiani.
Ndani ya gari lake kulikutwa na vilevi lukuki ikiwemo Wisky aina ya Bond 7 aliyokuwa anakunywa marehemu.
Mpenzi wake Jackline Joseph anashikiliwa na jeshi la polisi hadi hapo uchunguzi utakapokamilika, sababu ya kifo hicho bado haijafahamika.

Soma Nafasi za kazi na ajira bofya hapa chini kutizama, Mjulishe na mwenzio

Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio

Post a Comment

 
Top