Inawezekana mwaka 2014 ukawa mwaka mwingine ambao mastaa wengi wa Tanzania kuanzia kwenye movie, muziki na sekta nyingine wamehusika sana kwenye headlines za uchumba na ndoa.
Post hii ya leo ni maalum kwa ajili ya Mwanamitindo wa kimataifa anaetokea Tanzania Flaviana Matata ambae amekua akiishi Marekani, kafungua page mpya kwenye maisha yake baada ya kuvishwa pete ya Uchumba.
Kwa furaha aliyokua nayo, Flavvy aliipost picha kwenye page yake ya Instagram @FlavianaMatata Nov 16 2014 na kuionyesha hiyo pete na kama vile haitoshi, akaandika maneno ya ‘I said YES‘ ambapo Yes aliiandika kwa herufi kubwa…. yaani ‘Nilikubali au nilisema ndio’
Baada ya kujua kwamba sasa Flaviana Matata kavishwa pete tayari, kingine kinachosubiriwa ni kumjua shemeji.
Sifa mojawapo ya Flaviana Matata ni pamoja na kuingia kwenye list ya MillardAyo ya mastaa ambao ni Watanzania na wanaishi nje ya nchi lakini wamekua wakiikumbuka nchi yao na hurudi mara kwa mara kwa ajili ya kazi za kusaidia jamii walizozianzisha.
Headlines za Flavvy mara nyingi zimekua za kazi ya msaada anaoutoa mashuleni au kwa Wanafunzi kupitia Flaviana Matata Foundation.
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment