Msafara kuelekea kwenye msikiti mkuu wa
Ijumaa mjini Kahama kwa ajili ya mwili wa marehemu kuswaliwa mchana wa
leo ambapo mami ya watu kutoka ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga
wamejitokeza kumzika(Bibi Halima Nchimika amezaliwa mwaka 1940) mama
mzazi wa mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Khamis
Mgeja.Mazishi yamefanyika katika makaburi ya Uhindini mjini
Kahama.Wakati mwili wa marehemu ukitolewa nyumbani mvua ilianza kunyesha
muda mfupi ikakatika kabla ya kufikishwa msikitini,baada ya hapo
msafara ulielekea makaburini,mazishi yakaendelea,lakini wakati
yakielekea mwisho mvua ikanyesha na kusindikiza msafara hadi nyumbani
kisha ikakatika-Picha na Kadama Malunde
|
Mwili
wa marehemu ukiwasili katika makaburi ya Uhindini mjini Kahama leo
mchana,ambapo watu mbalimbali wenye mapenzi mema wakiwemo viongozi wa
serikali,vyama vya siasa,dini na wengine wengi wamejitokeza kumzika bi
Halima Nchimika(74) aliyefariki dunia jana wakati akipatiwa matibabu
katika hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza baada ya kuugua muda
mrefu-Picha na Kadama Malunde |
|
Mazishi
yanaendelea-Pia mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga alikuwepo(mwenye
suti nyeusi na miwani kushoto),kulia kwake ni katibu wa CCM mkoa wa
Shinyanga-Picha na Kadama Malunde |
|
Mazishi yanaendelea-Picha na Kadama Malunde |
|
Mtoto
wa marehemu ambaye ni mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja
akiweka udongo kaburini kumzika mama yake Halima Nchimika aliyefariki
dunia jana jijini Mwanza-Picha na Kadama Malunde |
|
Mstahiki
meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafidh Mukadam akiweka udongo
kaburini,nyuma yake ni Boniface Butondo mjumbe wa NEC taifa,akifuatiwa
na mbunge wa Kahama mjini James Lembeli-Picha na Kadama Malunde |
Mbunge wa Kahama mjini James Lembeli akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi leo mchana-Picha na Kadama Malunde
|
WAKATI MAZISHI YANAENDELEA MVUA IKANYESHA-,Pichani
ni msafara wa waombolezaji wakitoka makaburini kuelekea nyumbani kwa
Mgeja mtaa wa Nyasubi mjini Kahama huku mvua ikinyesha,ambapo wataalam
wa mambo walisema hiyo ni ishara ya marehemu kupokelewa na mungu -Picha
na Kadama Malunde |
|
Nyumbani
kwa mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga palipo na msiba,waombolezaji
wakiwa wamekaa baada ya mazishi kusubiri utaratibu mwingine-Picha na
Kadama Malunde |
Kushoto ni kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga SACP Justus Kamugisha akiwa msibani leo-picha na Kadama Malunde
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja katika mtaa wa Nyasubi mjini Kahama-Picha na Kadama Malunde
|
Sheikh wa mkoa wa Shinyanga Ismail Habibu Makusanya akizungumza baada ya mazishi-Picha na Kadama Malunde |
|
Mbunge
wa Msalala wilayani Kahama Ezekiel Maige ambaye ni mwenyekiti wa
wabunge wanane wa mkoa wa Shinyanga akitoa salamu za rambirambi kwa
niaba ya wabunge wenzake-Picha na Kadama Malunde |
Mbunge wa Msalala wilayani Kahama Ezekiel Maige akiteta jambo na mbunge wa Kahama mjini James Lembeli -Picha na Kadama Malunde
|
Mbunge wa Kahama mjini James Lembeli akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya wananchi wa Kahama-Picha na Kadama Malunde |
|
Mbunge
wa Kahama mjini James Lembeli(kushoto) akiwa amekumbatiana na
mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga baada ya kutoa salamu za rambirambi
na kumpa pole kwa kufiwa na mama yake mzazi-Picha na Kadama Malunde |
|
Mbunge wa Kishapu Suleiman Masoud Nchambi akizungumza baada ya mazishi nyumbani kwa Mgeja leo-Picha na Kadama Malunde |
|
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa Mgeja leo-Picha na Kadama Malunde |
Aliyeshikilia kipaza sauti(wa nne kutoka kushoto) ni Mjumbe wa halmashauri kuu CCM taifa Dkt Rafael Masunga Chegeni akiwa na wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM kutoka kanda ya ziwa nyumbani kwa Mgeja leo-Picha na Kadama Malunde
|
Mbunge
wa Shinyanga mjini Stephen Masele ambaye pia ni naibu waziri wa madini
nchini akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya serikali ya muungano wa
Tanzania leo-Picha na Kadama Malunde |
|
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa Mgeja leo-Picha na Kadama Malunde |
|
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindayi ambaye ni mwenyekiti wa wenyeviti
nchini akizungumza kwa niaba ya wenyeviti wenzake.pia alitoa salamu za
rambi rambi kutoka kwa mheshimiwa Edward Lowassa waziri mkuu
mstaafu,ambaye ni mbunge wa Monduli -Picha na Kadama Malunde |
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Singida Mgana Msindayi ambaye ni mwenyekiti wa wenyeviti
akimpa mkono wa pole mtoto wa marehemu( Khamis Mgeja )leo-Picha na Kadama Malunde
|
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akito neno la shukrani kwa watu
wote walioshiriki katika msiba huo-Picha na Kadama Malunde |
|
Waombolezaji wakiwa msibani leo-Picha na Kadama Malunde |
|
Waombolezaji wakiwemo viongozi wa dini wakiwa nyumbani kwa Mgeja leo-Picha na Kadama Malunde |
|
Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa Mgeja leo-Picha na Kadama Malunde |
|
Mjumbe
wa halmashauri kuu CCM mkoa wa Richard Masele Msanii(mwenye kofia
kushoto) aliyemwakilisha mbunge wa Jimbo la Solwa Ahmed Salum akiwa na
mkuu wa wilaya ya Kahama ndugu Benson Mpesya,nyuma yao ni meneja wa
Kahama Fm ndugu Marco Mipawa-Picha na Kadama Malunde |
|
Baada
ya mazishi -Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika picha ya pamoja na
mwenyekiti wa ccm mkoa wa Shinyanga,wa kwanza kulia ni mkurugenzi wa
Malunde1 blog,ndugu Kadama Malunde-Picha na Mohab Dominic |
|
Waandishi
wa habari nao walikuwepo,wa kwanza kushoto ni Mohab Dominic gazeti la
Nipashe,katikati ni Chibura Makorongo mwandishi wa habari gazeti la
Uhuru na Mzalendo,akifuatiwa na Kadama Malunde mwandishi wa gazeti la
Mtanzania pia mkurugenzi wa Malunde1 blog.Waandishi wengine hawako
pichani ambao ni Raymond Mihayo gazeti la Habarileo na Ali Lityawi
gazeti la Tanzania Daima na Ndalike Sonda kutoka Radio Kahama-Picha na
Ndalike Sonda |
Post a Comment