Football - International Friendly - South Africa v Senegal - Moses Mabhida Stadium - Durban
Michezo kadhaa ya kufuzu kwa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika imefanyika hii leo Novemba 15 katika viwanja tofauti barani.
Michezo hiyo ambayo ni ya pili kutoka mwisho katika hatua ya makundi ya kufuzu imetoa timu kadhaa ambazo zimefuzu kushiriki michuano ya AFCON ambayo itafanyika nchini Equatoria Guinea.
Katika michezo hiyo timu ya taifa ya Afrika Kusini ‘Bafana Bafana’ imefanikiwa kufuzu baada ya kuwafunga Sudan katika mchezo uliopigwa jijini Durban kwenye uwanja wa Moses Mabhidha .
Afrika kusini ilishinda mchezo huo kwa matokeo ya 2-1 kufuatia mabao yaliyofungwa na Thulani Serero na Tokelo Rantie . Sudan walijipatia bao lao pekee kwenye dakika ya 76 mfungaji akiwa Salah Ibrahim ambaye aliingia kwenye kipindi cha pili.
Afrika kusini wamefanikiwa kufuzu kama washindi wa makundi baada ya kukusanya pointi 11 kutokana na kushinda mechi 3 na kutoka sare kwenye mechi mbili, huku kundi ‘A’ timu ya taifa ya Nigeria ilifanikiwa kuwafunga Congo Brazaville 2-0 katika mchezo uliofanyika Port Noire .
Matokeo haya yanawafanya Nigeria kufikisha pointi 7 sawa na walizo nazo Congo Brazzavile na Nigeria watalazimika kungoja mpaka siku ya mwisho ya kufuzu ili kujihakikishia nafasi ya kutetea ubingwa wao kwani watategemea matokeo ya mchezo kati ya Congo Brazzavile na Sudan.
Katika michezo mingine Cameroon waliwafunga Congo DRC 1-0, huku Ivory Coast wakiwafunga Sierra Leone 5-1 . Gabon na Angola walitoka sare ya 0-0 na Burkina Faso wakashinda mchezo wao dhidi ya Lesotho kwa 1-0, Zambia ambao walikuwa ugenini Msumbiji walishinda mchezo wao dhidi ya wenyeji kwa matokeo ya 1-0 kwa bao lililofungwa na mshambuliaji wa Tp Mazembe Given Singuluma.
Uganda waliwafunga Ghana 1-0 matokeo ambayo yanawafanya washike nafasi ya pili kwenye kundi lao na kwa matokeo haya timu za Afrika Kusini , Cameroon , Tunisia , Burkina Faso , Algeria , Gabon , na Cape Verde zimeungana na wenyeji Equatorial Guinea kama timu zilizofuzu huku timu nyingine zikilazimika kungoja mpaka siku ya mwisho ya michezo ya kufuzu ili kukata tiketi ya kwenda huko Malabo ambako michuano ya Afcon 2015 itafanyika.

Soma Nafasi za kazi na ajira bofya hapa chini kutizama, Mjulishe na mwenzio

Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio

Post a Comment

 
Top