8164_top_story
Zoezi la utoaji wa Vitambulisho vya Uraia limeendelea leo, kituo cha Televisheni TBC1 kimeripoti kuhusu namna zoezi hilo lilivyofanyika.
Katika taarifa hiyo baadhi ya watu waliohojiwa maeneo ya Sinza wameongelea kuhusu hilo, mmoja wa watu hao Chiku Abdalla amesema; “….Utaratibu ni mbovu, kwa hiyo kwa mtazamo wangu mimi kama mimi..wangefanya utaratibu kwamba Sinza C wachukulie Serikali ya mtaa C, D, E na A… yaani kila mtaa ukachukulie kwenye Serikali yake ya mtaa…
Naye Abbas Mohamed amesema; “..Sasa zoezi lirudi Serikali za mtaa sio kata kama hawana vifaa waongezewe vifaa… Halafu mimi nauliza, kitambulisho kina miaka kumi, ina maana mimi uraia wangu miaka kumi…
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Sinza ‘A’ na Sinza ‘B’, Ibrahim Mabewa amesema; “… Kwenye kata kama hizi ambazo zina changamoto ni vizuri wakarudisha mpaka kule kwenye mitaa.. ili kila mmoja akawajibike kwenye mtaa wake.. naamini inaweza ikapunguza hizi changamoto za vurugu na mambo haya, vinginevyo tuhuma za wananchi haziwezi kuisha..

Soma Nafasi za kazi na ajira bofya hapa chini kutizama, Mjulishe na mwenzio

Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio

Post a Comment

 
Top