Kijana ambaye hakuweza kufahamika jina lake mapema, akiugulia maumivu baada ya kupokea kichapo kutoka kwa wananchi wenye hasira kwa kile walichomtuhumu kuiba simu katika moja ya duka lililopo maeneo ya Makumbusho karibu na Kituo cha Daladala, jijini Dar es Salaam. 

Wakielezea tukio hilo mashuhuda walisema kuwa kijana huyo aliingia katika duka hilo lililokuwa na mwanadada na kupora simu iliyokuwa juu ya kabati la bidhaa na kutimka nayo jambo lililomfanya mwanadada huyo kutoka nje na kuanza kupiga kelele za kuomba msaada. 

Kama ilivyo kawaida kijana huyo aliangushiwa na kila mtu aliyemuona akitimka na kufanikiwa kumtia nguvuni na kuanza kula kichapo hadi aliporejesha simu ya mdada huyo. Baadaye aliachiwa huru na kuondoka zake.

 Kijana huyo akijificha chini ya ua akihisi kuwa hapo ni mahala salama kwa wakati huo baada ya kula kichapo....
 Akipiga kelele na mayowe kuomba msamaha asiendelee kula kichapo
Akimng'ang'ania kijana akiyemuokoa ili amsindikize kutoa eneo hilo lenye ngumi za moto kuliko maelezo...

Soma Nafasi za kazi na ajira bofya hapa chini kutizama, Mjulishe na mwenzio

Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio

Post a Comment

 
Top