Staa wa Filamu za Kibongo, Yvonne Sherry ‘Monalisa’ hivi karibuni aliweka wazi kuwa anatamani kuolewa lakini hajampata wa kumuoa.Monalisa alifunguka maneno hayo baada ya uvumi kuenea kuwa amepata mtu anataka kumuoa na mipango ya ndoa iko tayari.
   Staa wa Filamu za Kibongo, Yvonne Sherry ‘Monalisa’.

“Mh! Wewe si wa kwanza kuniambia maneno haya jamani hivi yanatoka wapi? Mimi sijapata mtu wa kunioa jamani ila nikimpata nitaolewa kwa sababu jua limekuchwa pia ndoa ni jambo la heri,” alisema Monalisa

Katikati ya mwaka huu, Monalisa alionyesha matamanio yake ya ndoa ambapo alivaa shera kwenye harusi ya rafiki yake na kuingia na mumewe ikiwa kama maigizo kituko hicho kiliipendezesha shughuli hiyo

Soma Nafasi za kazi na ajira bofya hapa chini kutizama, Mjulishe na mwenzio

Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio

Post a Comment

 
Top