Mkuu
wa Wilaya ya Korogwe,mkoani Tanga Mrisho Gambo, ameliagiza Jeshi la
Polisi na Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, Lucas Mweri,
kumchukulia hatua daktari anayetuhumiwa kumbusu mgonjwa wake wakati
akimtibu.
Gambo
alitoa agizo hilo jana baada ya kupokea malalamiko ya tukio hilo na
kueleza kuwa ni la ukiukwaji wa maadili ya kidaktari na aibu kwa wilaya.
Aliliagiza
jeshi la polisi kufanya uchunguzi na kuchukua hatua za kisheria ili iwe
fundisho kwa mtaalamu huyo na wengine wenye tabia kama hiyo.
Awali
ilidaiwa kuwa daktari huyo, Ally Naah anayefanyakazi Hospitali ya
Wilaya ya Korogwe ya Magunga, anadaiwa kumbusu mwanamke aliyekwenda
kupata matibabu hospitalini hapo.
Mashuhuda
wa tukio hilo walisema siku ya tukio mwanamke huyo aliambatana na
mumewe hadi hospitalini hapo kwa ajili ya kupata matibabu na baada ya
kufika daktari huyo alimtaka aingie ndani kumfanyia uchunguzi.
Ilidaiwa
kuwa, mume wa mwanamke huyo aliyekuwa nje akimsubiri mkewe alipata
hofu baada ya kuona muda mrefu umepita bila mkewe kutoka, ndipo
alipochungulia dirishani na kumuona daktari huyo akimbusu.
“Yule
bwana hakuamini alichokiona, hakuvumilia na alipiga kelele akiomba
msaada…Kwa kweli jambo hili ni aibu na limetuondolea uaminifu,” alisema
mmoja wa shuhuda wa tukio hilo.
Hata
hivyo, habari za kipolisi zinaeleza kuwa tayari tukio hilo limeshaanza
kufanyiwa kazi ikiwamo kufuatiliwa eneo lilipotendeka kosa hilo kwa
hatua zaidi za kisheria.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Dk Olden Ngasa, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema mtuhumiwa alitoroka baada ya tukio hilo.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Dk Olden Ngasa, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema mtuhumiwa alitoroka baada ya tukio hilo.
NA DEGE MASOLI
Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio
Post a Comment