s2
.
Kwenye hii picha ya kwanza inaonekana sehemu ya kupaki pikipiki aina ya Bajaji ambapo kibao chake kimezibwa kuzuia bajaji zisiingie ndani, kwenye siku ya kwanza bajaji zilikuwa zinaingia ndani na kulipa sh.500 kila wakitoka na abiria ila ilipofika mida ya mchana walikatazwa kuingia ndani.
Kwa taarifa zilizotoka kwa uongozi wa kituo hicho siku kadhaa zilizopita ni kwamba wanapanga utaratibu maalumu na watazisajili bajaji 20 tu ambazo zitaruhusiwa kuingia ndani.
Ni kituo kipya cha Mabasi ambacho kimechukua nafasi ya kile kidogo cha Ubungo kilichokuwepo karibu na TANESCO, hiki kipya kilichopo Sinza kilianza kufanya kazi October 23 2014.
s1
s3
Baadhi ya madereva wa bajaji wakiwa wameegesha bajaji zao nje huku wakiwa wanajadili hatima yao itakuwaje jinsi ya kubeba abiria katika kituo hiko.
s4
Wengi wa abiria walikuwa wanalalamika kutokana na mabasi mengi kutokufika katika eneo hilo hivyo usafiri ulikuwa mgumu.
s5
s6
s7
Hiki ni kituo kipya cha polisi kilichopo ndani ya stand hii.
s8
Askari wa usalama barabarani wakiwa kazini ndani ya kituo hiki kipya
s9
Taa za kituo cha mabasi Sinza ambazo zinawaka kwa kutumia nguvu ya Jua, baadhi ya watu ambao huwa maeneo hayo usiku wanasema ikifika saa tano usiku huwa zinazima, kituo cha polisi kina umeme wa tanesco.

Soma Nafasi za kazi na ajira bofya hapa chini kutizama, Mjulishe na mwenzio

Facebook Blogger Plugin by Bongo na Matukio

Post a Comment

 
Top